SAKAJA AJITENGA NA UHUNI NAIROBI
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amemtaka kamanda wa polisi eneo la Nairobi George Sedah kuwahakikishia ulinzi wa kutosha wakenya watakaoshiriki maandamano Jumatano hii, huku akijitenga na taarifa kwamba aliwafadhili wahuni kuwahangaisha waandamanaji na wapita njia jijini Nairobi wiki jana.
Aidha, Sakaja amewataka polisi kuwakamata watu waliohusika na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano hayo.
Haya yanajiri huku baadhi ya wakenya wakipanga maandamanao kuwakumbuka wenzao waliofariki kwenye maandamano ya tarehe 25 mwezi Juni mwaka jana.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































