#Local News

POLISI WARUDISHIWA MZIGO WA MAUAJI

Idara ya polisi imekabidhiwa mzigo wa kuwaambia wakenya ni nani aliyemuua bloga Albert Ojwang alipokuwa mikononi mwa polisi, baada ya ripoti ya upasuaji wa maiti kuonyesha kuwa Ojwang aliuawa na wala hakujiua jinsi Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja alivyodai.

Kulingana na mpasuaji wa serikali Bernard Midia, Ojwang alipigwa, kuteswa na kuonyesha dalili za kunyongwa, tofauti na madai ya polisi kwamba alijiua kwa kugongesha kichwa chake kwenye ukuta wa seli za polisi.

Babake bloga huyo Meshack Ojwang, sasa ametaka naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kuwajibishwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

POLISI WARUDISHIWA MZIGO WA MAUAJI

DIG LANGAT CHINI YA SHINIKIZO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *