MAHANGAIKO ZAIDI VYUONI KUFUATIA MGOMO
Shughuli za masomo zimeendelea kutatizika katika vyuo vikuu vya umma nchini kwa wiki ya 4 sasa kufuatia mgomo wa wahadhiri ambao hii leo wameandamana jijini Nairobi na kuelekeza malalamishi yao katika majengo ya bunge, wizara ya fedha na ile ya elimu.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano wa UASU Daktari Constantine Wasonga na mwenyekiti Grace Nyongesa, wahadhiri hao wameshikilia kuwa hawatarejea kazini hadi maslahi yao yatakatapotimizwa.
Miongoni mwa malalamishi yao ni nyongeza ya mishahara, bima ya afya na kuajiriwa kwa wafanyakazi Zaidi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































