GACHAGUA APATA PIGO MAHAKAMANI, HOJA DHIDI YAKE KUENDELEA

Naibu rais Rigathi Gachagua amepata pigo baada ya mahakama kudinda kuzuia bunge kusitisha mchakato wa kumbandua kutoka afisini.
Kesi hiyo imewasilishwa na aliyekuwa seneta wa Kakamega Cleophas Malala, akitaka mahakama izuie kuwasilishwa bungeni na kujadiliwa kwa mswada huo kwa misingi kwamba bunge la kitaifa na lile la seneti hayajaafikia usawa wa kijinsia kuendesha kikao hicho.
Hata hivyo, jaji Bahati Mwamuye amepuzilia mbali ombi hilo, kesi hiyo ikiratibiwa kutajwa tarehe 7 Oktoba.
Wakati uo huo, baadhi ya wkaenya sasa wanaunga mkono hatua ya wabunge kutaka kumwondoa naibu huyo wa rais mamlakani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa