ILINIVUNJA MOYO SANA
Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala amefunguka kuhusu kushindwa kwake kufika fainali ya mbio za 100m kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, akisema kuwa ‘amehuzunika sana’ lakini akahakikisha kwamba hilo halitaharibu kazi yake.
Omanyala aliondolewa katika nusu fainali huku Noah Lyles akisonga mbele na kushinda medali ya kwanza ya dhahabu kwa USA tangu 2004, akitumia sekunde 9.77.
Bingwa huyo wa Michezo ya Jumuiya ya Madola hata hivyo alisema amejifunza mambo mengi mazuri mjini Paris na atarejea kwa kishindo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































