WASHUKIWA WA MAUAJI YA WERE KUCHUNGUZWA

Washukiwa 2 wa mauaji ya mbunge wa Kasipul Charles Were watafanyiwa uchunguzi wa akili kabla ya kufunguliwa mashtaka, kufuatia agizo la mahakama.
Jaji Magret Muigai ameagiza Isaack Kuria na Allan Omondi Ogolla wafanyiwe uchunguzi huo na kuzuiliwa katika gereza la Kamiti.
Were aliwawa kwa kupigwa risasi mwezi Aprili Nairobi na mshukiwa aliyetoweka kwa kutumia pikipiki.
Imetayarishwa na Maureen Makhobe