#Business

IMF HUENDA IKAIDHINISHA MPANGO MPYA WA FEDHA WA KENYA AGOSTI – MUDAVADI

Kenya imewasilisha mpango mpya wa kifedha kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) baada ya maandamano ya wiki nzima nchini kote kulazimisha Rais William Ruto kuondoa Mswada wa Fedha wa 2024.

Mswada huo tata ambao umezusha wimbi la maandamano nchini umependekeza hatua kadhaa mpya za ushuru ambazo zingeweza kuifanya serikali kukusanya angalau Shilingi bilioni 347 kufadhili bajeti ya 2024/25.

Sheria iliyopendekezwa ilioanishwa na masharti ya kifedha ya IMF kwa Kenya, haswa katika ujumuishaji wa ndani, ikilenga kupunguza deni kubwa la nchi.

Wiki iliyopita, Hazina ya Kitaifa ilieleza mipango ya kupunguza matumizi ya mwaka 2024/25 kwa asilimia 1.9 na kupanua nakisi ya fedha hadi asilimia 3.6 ya Pato la Taifa, hivyo kulazimika kukopa zaidi.

Uchumi mkubwa zaidi wa Afrika Mashariki sasa unapanga kufadhili bajeti ya trilioni 3.8 kwa mwaka ulioanza Julai 1 kushuka kutoka trilioni4.2 za awali.

Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi ambaye alifika mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti siku ya Jumatatu alisema Kenya inatarajia bodi ya hazina hiyo kuipitia ili kuidhinishwa mwishoni mwa mwzi ujao wa Agosti.

Kauli hiyo inajiri wakati uhusiano wa Kenya na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ukiwa chini ya uangalizi mkali, huku wananchi wakilaumu chama hicho kwa kuishinikiza serikali kuongeza ushuru.

Wiki iliyopita, Taasisi ya Masuala ya Kiuchumi (IEA) ilishutumu Hazina kwa kubadilisha lengo lake la ujenzi mpya wa kifedha wa Kenya, na kuongeza hali zaidi ambazo ni hatari kwa uchumi.

Imetayarishwa na Janice Marete

IMF HUENDA IKAIDHINISHA MPANGO MPYA WA FEDHA WA KENYA AGOSTI – MUDAVADI

HATUFADHILI MAANDAMANO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *