MPAKA HURU AFRIKA NI MUHIMU KWA UKUAJI WA UCHUMI

Vuguvugu la afrikan Rising Unity Justice and Peace linaendelea kushinikiza umuhimu wa kuwa na mpaka uhuru barani afrika.
Kulingana na vuguvugu hilo, hili litawezesha mataifa wanachama kujistawisha kiuchumi kupitia upatikanaji wa soko pana na huru kwa bidhaa zinazokuzwa na kuzalishwa barani afrika.
Afisa wa mawasiliano wa vuguvugu hilo Ann Njagi amesema hali hiyo vile vile itachangia uhamasishaji wa ujuzi kutoka kwa raia hadi rai ana kutoka taifa hadi taifa..
Njagi amesema wakati umefika wa kushinikizwa kuwa na sarafu ya Pamoja barani afrika.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































