RUTO ANYIMWA NAFASI KULIHUTUBIA BUNGE LA MAREKANI

Rais William Ruto hatahutubia kikao cha pamoja cha Congress katika ziara yake ijayo ya Kiserikali nchini Marekani.
Hii ni baada ya Spika Mike Johnson kukataa ombi la baadhi ya wabunge wa Democrat waliokuwa wamemwalika Rais Ruto kuhutubia bunge la kitaifa la marekani.
Katika taarifa naibu mkuu wa wafanyikazi wa Spika Johnson Raj Shah amesema uamuzi wa kutomwalika Ruto kuhutubia kikao cha pamoja cha bunge umetokana na vikwazo vya kuratibiwa.
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































