#Football #Sports

KESI YA KUSIKIKIZWA KWA MASHTAKA DHIDI YA MANCHESTER CITY YA UKIUKAJI WA KANUNI ZA FEDHA TAYARI IMEANZA

Kesi ya kusikilizwa kwa mashtaka dhidi ya Manchester City kwa madai ya kukiuka kanuni za fedha za Ligi Kuu ya Uingereza tayari imeanza.

City walishtakiwa mnamo Februari 2023 kufuatia uchunguzi wa miaka minne. Inadaiwa timu hiyo ilikiuka sheria za kifedha kati ya 2009 na 2018. Wamekanusha mashtaka yote.

Usimamizi wa ligi ya Uingereza, EPL, unadai City ilikiuka sheria zinazohitaji klabu kutoa taarifa sahihi za kifedha kama vile mapato ya klabu.

Pia umewashutumu mabingwa hao wa Ligi kuu kwa kudinda kushirikiana na wapekuzi kwenye uchunguzi.

Yakijiri hayo, mkufunzi wa City Pep Guardiola aliwasihi wachezaji wa timu hiyo kutobabaishwa na kesi inayokumba klabu hiyo huku akionyesha matumaini kuwa suluhu mwafaka itapatikana.

Imetayarishwa na Kennedy osoro

KESI YA KUSIKIKIZWA KWA MASHTAKA DHIDI YA MANCHESTER CITY YA UKIUKAJI WA KANUNI ZA FEDHA TAYARI IMEANZA

TETESI ZA SOKA ULAYA- KLABU YA CRYSTAL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *