WANANDOA WAZEE WAUAWA KATIKA KISA CHA MOTO LARI, LIMURU

Polisi wanachunguza kisa ambapo wanandoa wazee waliuawa kwenye kisa cha moto eneo la Lari, Limuru, Kaunti ya Kiambu.
Miili ya Peter Kimani Kuria mwenye umri wa 75 na mkewe Miriam Muthoni 65, ilipatikana muda mrefu baada ya nyumba yao ya vyumba vitatu kuezekwa.
Wenyeji katika kijiji cha Lare wameripoti kuwa kulikuwa na moto katika nyumba hiyo yenye vyumba vitatu.
Moto ulikuwa umeteketeza nyumba nzima. Baadaye ilibainika kuwa wanandoa hao walichomwa moto kiasi cha kutotambulika.
Kamanda wa polisi kaunti ya Kiambu Michael Muchiri akithibitisha kisa hicho amesema wataalamu wataeleza zaidi kuhusu chanzo cha moto huo baada ya uchunguzi kukamilika.
Mabaki ya miili hiyo yamepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kusubiri uchunguzi.
Imetayarishwa na Janice Marete