MAGAVANA WALALAMIKIA UKOSEFU WA FEDHA
Magavana wameitaka serikali kuu kutoa mgao wa kaunti wa miezi ya Februaria na Machi mwaka huu ili kuwawezesha kuendeleza utoaji huduma kwa wakazi wanazoesema zimeathirika kutokana na ukosefu wa fedha.
Kwa mujibu wa gavana wa Kakamega Fernandez Barasa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya fedha katika baraza la magavana, kaunti zinaidai serikali kuu shilingi bilioni 63 za kipindi hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































