CHERUIYOT KIRUI AMEAGA DUNIA KATIKA MLIMA WA EVEREST
Mkenya mmoja Cheruiyot Kirui aliyeripotiwa kutoweka alipokuwa akipanda mlima Everest ulioko barani Asia ameaga dunia.
Mwili wa kirui umepatikana mita chache tu kutoka kilele cha mlima huo ,aidha shughuli ya kumtafuta mwongozaji wake Sherpa Nawang zingali zinaendelea.
Kirui na Nawang walikuwa katika msafara ulioandaliwa na seven summit Tricks SST wenye makao wenye makao yake Kathmandu Nepal walipoteza mawasiliano na kikosi chao walipokuwa wakijaribu kupanda katika kilele cha Bishop Rock kilichoko umbali wa mita elfu 8 katika mlima huo wa Everest.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa SST Mingma Sharpa wawili hao walianza safari hiyo bila kutumia Oxygeni ya ziada swala ambalo ni muhimu hata kwa wapandaji wenye uzoefu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































