KAULI YA MAWAZIRI KUHUSU BAJETI
Baraza la mawaziri limetetea bajeti ya shilingi trilioni 3.91 ya mwaka wa kifedha wa 2024-25 likisema imeratibiwa kufanikisha utekelezaji wa ajenda ya serikali ya Bottom up.
Katika taarifa baada ya kikao cha baraza hilo, limesema mojawapo ya masuala yatayopewa kipaumbele ni kuafikia usawa wa kiuchumi na kijamii, ikiwemo afya kwa wote, elimu, maji safi na utoshelezi wa chakula.
Aidha, taarifa hiyo imesema bajeti hiyo inalenga kuhakikisha usawa wa kimaendeleo na kukuza ugatuzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































