#Local News

MASWALI YA DCI KWA KETER

Mbunge wa zamani wa Nandi Hills Alfred Keter amehojiwa wa makachero wa idara ya upelelezi DCI katika makao makuu ya idara hiyo, akifichua kwamba ametakiwa kuweka wazi uhusiano uliopo baina yake na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Akizungumza na wanahabari baada ya kuhojiwa, Keter aidha, amesema ameulizwa kuhusiana na Sakata za bunduki kutoka taifa la Kongo, akihusisha kuhangaishwa kwake na njama ya serikali kuwanyamazisha wanaoikosoa.

Aidha, Keter ambaye alikamatwa hapo jana na kuachiwa huru, amesema masaibu yake yametokana naye kuzungumzia masuala yanayolikumba taifa, na kuapa kuendelea na azma yake ya kukosoa serikali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *