KENYA YAPATA UFADHILI WA DOLA BILIONI 3.6

kenya imepata ufadhili wa dola bilioni 3.6 yaani shilingi bilioni 477 za kenya kutoka marekani zitakazofanikisha ujenzi Express Way kutoka Nairobi hadi Mombasa.
Barabara hiyo itaunganisha mji mkuu wa Nairobi na Mombasa hatua ambayo itaimarisha shughuli ya miji hiyo miwili yenye shughuli nyingi.
Makubaliano baina hya kenya na kampuni ya evestrong capital LLC yalitiwa Saini na mamlaka ya ujenzi wa barabara kuu KENHA hapo jana wakati wa ziara yar ais Ruto nchini marekani.
Uekezaji huo ujtasimamiwa na taasisi za klifedha za marekani kwa ushirikiano na sekta za binafsi nchini.
Imetayarishwa na Janice Marete