#Local News

MSHUKIWA WA MAUAJI ANA MATATIZO YA KIAKILI, RIPOTI

Juhudi za kusaka haki kwa familia ya Sylvia Kemunto ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Multimedia zimepata pigo baada ya kubainika kuwa mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanafunzi huyo Eric Mutinda hayuko sawa kiakili na hivyo kesi ya mauaji dhidi yake haiwezi kuendelea kwa sasa.

Hii ni kufuatia ripoti ya uchunguzi wa kiakili uliofanywa katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Mathari, ikionyesha kuwa Mutinda ana matatizo ya akili.

Hata hivyo, mahakama imeamuru kwamba idara ya magereza imrejeshe hospitalini humo kufanyiwa uchunguzi upya, kesi hiyo ikirataibiwa kutajwa Ijumaa wiki hii.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *