MIHEMKO YA UHAMISHO KATIKA LIGI KUU YA UINGEREZA
Bayern Munich wanafikiria kumnunua Marcus Rashford, Arsenal wanakaribia kumnunua Viktor Gyokeres, Crystal Palace wakubali bei ya pauni milioni 47 kwa Ousmane Diomande.
Bayern Munich wanafikiria kumnunua fowadi wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, baada ya kufurahishwa na kiwango chake cha mkopo Aston Villa msimu uliopita.
Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres. Mchezaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 27 ameiambia klabu yake kuwa anataka kujiunga na The Gunners.
Crystal Palace wamefikia makubaliano ya pauni milioni 47 kumsajili Ousmane Diomande, 21, kutoka Sporting huku beki huyo wa Ivory Coast akionekana kama mbadala wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Marc Guehi, 24.
Manchester United wamewasiliana na Inter Milan kuhusu dili la kumsaini kiungo wa kati wa Italia Davide Frattesi, 25.
Arsenal tayari wamewasilisha ofa kwa winga wa Uingereza Noni Madueke, 23, ambaye huenda akaondoka Chelsea msimu wa joto.
Juventus wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili fowadi wa Kanada Jonathan David, 25, ambaye mkataba wake uliisha Lille mwishoni mwa msimu uliopita.
Mshambulizi wa Colombia Jhon Duran, 22, anasafiri kwa ndege kutoka nyumbani kwao hadi Uturuki kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Al-Nassr hadi Fenerbahce.
Newcastle wanahaha kumnunua beki wa kati wa Marseille na Argentina Leonardo Balerdi, 26, ambaye pia anavutia Juventus.
Burnley wanafanyia kazi chaguzi za mshambuliaji kwa meneja Scott Parker huku fowadi wa Genk na Nigeria Tolu Arokodare, 24, akizingatiwa.
AC Milan wanatumai kumsajili kiungo wa kati wa Uswizi Ardon Jashari, 22, kutoka Club Brugge kwa mkataba wa takriban £30m.
Manchester City itamsajili kinda wa miaka 15 Caelan-Kole Cadamarteri kutoka Sheffield Wednesday kwa mkataba wa £1.5m. Fowadi huyo ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Everton Danny.
West Ham wanakabiliwa na vita vya kumshawishi Slavia Prague kumuuza beki wa kushoto wa Senegal El Hadji Malick Diouf, 20.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































