RICE ASEMA WATAWAPIKU UHOLANZI

Declan Rice ana imani wana uwezo wa kuibwaga Uholanzi katika nusu fainali na hatimaye kunyakua ubingwa wao wa kwanza wa ulaya.
Kiungo huyo wa kati wa Arsenal amekuwa nguzo ya Uingereza toka makala haya kuanza lakini anjihisi mtulivu kuelekea mechi ya leo mjini Dortmund, lakini anatarajia mchezo mgumu.
Takwimu zinaonyesha wazi mchango wa Rice kwa Uingereza, kwani amekimbia umbali wa kilomita 63.9 (maili 39.7), umbali mrefu zaidi kuliko mchezaji yeyote wa timu hiyo kwa mechi tano, huku akiwa wa nne wa kukaba na kupokonya mipira wapinzani.
Ushindi huko Dortmund utaipeleka England hadi fainali ya pili mfululizo ya Euro na fainali yao ya tatu kuu kwa jumla.
Imetayarishwa na Nelson Andati