JADON SACHO AREJEA MACHESTER UNITED
Chelsea imeamua kutomsajili winga Jadon Sancho kwa mkataba wa kudumu na badala yake italipa ada ya pauni milioni 5 ili kumrudisha mchezaji huyo Manchester United.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza alihamia Stamford Bridge kwa mkopo msimu uliopita wa joto baada ya uhusiano wake na meneja wa zamani wa United Erik ten Hag kuvunjika.
United, ambao walimsajili Sancho kwa £73m kutoka Borussia Dortmund mnamo 2021, wanataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aondoke.
Chelsea haikulipa ada ya mkopo kwa mchezaji huyo na ililipa nusu tu ya mshahara wake wa pauni 300,000 kwa wiki.
The Blues walikuwa wamekubali wajibu wa kumnunua Sancho kwa ada ya takriban 25m ikiwa wangemaliza nafasi juu ya nambari 14 kwenye Premier League, jambo ambalo walifanya – au kulipa ili kujiondoa kwenye mpango huo.
Hata hivyo, klabu hiyo na wawakilishi wa mchezaji huyo hawajaweza kuafikiana kuhusu mkataba wa Sancho, ambaye angelazimika kukatwa mshahara kutokana na mkataba wake na United.
Mchezaji huyo wa Uingereza amebakiza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake ya United, na klabu bado inadaiwa pauni milioni 17 na Dortmund.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































