#Football #Sports

WANJALA AJIUNGA NA ATHLETIC CLUB

Beki wa Kenya anayeimarika kwa kasi, Amos Wanjala amejiunga na klabu ya Athletic Club Torrellano inayoshiriki ligi ya daraja la tano nchini Uhispania.

Wanjala umaarufu wake umekuwa ukiongezeka tangu mwaka jana alipohamia Uhispania pamoja na Aldrine Kibet na Alvin Kasavuli pamoja na Vijana wengine kadhaa wa Kenya.

Watatu hao walijiunga na Nastic Sports Academy kufuatia onyesho lao la kuvutia wakiwa na Shule ya Upili ya Wavulana ya St. Anthony, timu ya kandanda ya Kitale iliyotwaa tena taji la kitaifa Agosti mwaka jana.

Beki huyo mahiri aliiongoza timu ya taifa ya walio na umri chini ya 18 U18 hadi kumaliza katika nafasi ya pili wakati wa mashindano ya CECAFA yaliyofanyika Desemba mwaka jana mjini Kisumu.

Wanjala, ambaye mara nyingi hucheza kama mlinzi wa kati, lakini amedhihirisha uhodari wake kwa kucheza pia kama beki wa kulia na kiungo mkabaji huko Uhispania.

Timu aliyojiunga nayo ya AC Torrellano ilianzishwa mwaka wa 2012 na huandaa mechi zao katika Uwanja wa Campo Municipal Isabel Stadium.

Imetayarishwa na Nelson Andati

WANJALA AJIUNGA NA ATHLETIC CLUB

KINERO NDO KOCHA WA MOMBASA UNITED.

WANJALA AJIUNGA NA ATHLETIC CLUB

ADAM AANDIKA HISTORIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *