WAPEENI WACHEZAJI WA NSL NAFASI KWA TIMU YA TAIFA

Siku chache baada ya kukamilika kwa msimu wa Ligi Kuu ya Kitaifa wa 2024/25, kocha msaidizi wa Klabu ya Soka ya 3K Moses Munene ametoa changamoto kwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanaume Bennie McCarthy kutafuta talanta kutoka kwa ligi ya daraja la pili.
Akielezea NSL kuwa ligi yenye ushindani mkubwa zaidi nchini, Munene aliteta kuwa NSL imejaa vipaji vya hali ya juu vinavyostahili kutambuliwa na inafaa kupewa nafasi katika timu ya taifa, Harambee Stars.
Wito wake umekuja wakati taifa likijiandaa kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka huu pamoja na Uganda na Tanzania mwezi Agosti.
Hata hivyo, hata Munene akitoa wito kwa timu ya taifa kuangaziwa, Ligi Kuu ya Kitaifa inaendelea kukabiliwa na changamoto za kifedha, huku mtaalamu huyo akitaka Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kupata mfadhili wake.
Imetayrishwa na Nelson Andati