LUSAKA ATETEA AKAUNTI ZA BENKI BUNGOMA

Gavana wa Bungoma Ken Lusaka ameihakikishia kamati ya ugatuzi katika bunge la seneti kwamba akaunti 352 za benki zilizofunguliwa na serikali yake ziliidhinishwa na msimamizi wa bajeti na benki kuu kabla ya kuanza kutumika.
Akizungumza alipofika mbele ya kamati hiyo, Lusaka amekiri kuwepo kwa akaunti hizo, akisema nyingi ya kaunti hizo zinaendeshwa na taasisi za elimu ya kiufundi kwenye kaunti hiyo, na kusema kwamba yuko tayari kushirikiana kwenye ukaguzi wa akaunti hizo.
Kwa mujibu wa Lusaka, taasisi hizo zina akaunti 152, huku vituo vya afya vikimiliki akaunti 146, na nyingine zinaendeshwa na hazina mbali mbali za kaunti hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa