RUTO AANZISHA MCHAKATO WA KUBUNI IPOA

Rais William Ruto ameteua kamati yenye wanachama 6 watakaowahoji wakenya wanaolenga kujaza nafasi ya mwenyekiti na wanachama 7 katika tume huru ya kuchunguza mienendo ya polisi IPOA.
Sita hao ni Arthur Osiya, Msagha Mbogoli, Joyce Nyabuti, Monica Muiru, Raymond Nyeris na Caroline Naikena, Rais akiwahimiza wakenya kutuma maombi ya kujaza nafasi hizo.
Walioteuliwa kubuni kamati hiyo ya usajili wanawakilisha idara mbali mbali za serikali ambazo ni afisi ya Rais, Idara ya mahakama, tume ya utumishi wa umma, tume ya EACC, tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu na ile ya jinsia na usawa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa