WAKENYA 316 WAMEFARIKI KATIKA MATAIFA YA GHUBA TANGU 2002 – MUDAVADI
Waziri Mkuu wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi amesema kuwa takriban Wakenya 316 wamefariki wakifanya kazi katika mataifa ya Ghuba tangu 2002 hadi sasa.
Akizungumza alipofika mbele ya kikao cha Seneti leo Jumatano, Mudavadi alisema wamesambaa katika majimbo sita kati ya manane.
Mataifa hayo ni pamoja na Saudi Arabia yenye vifo 166, Qatar 58, Falme za Kiarabu (UAE) 51, Iraq 25, Bahrain 10, Kuwait 6, huku Oman na Iran zikiwa na vifo sifuri.
Mudavadi alibaini kuwa Wakenya 416,548 hivi sasa wanafanya kazi katika majimbo haya alisema kati ya hao, Saudi Arabia ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya Wakenya 310,266.
Qatar ni ya pili kwa kuwa na wakenya 66,025, na UAE ya tatu ikiwa na Wakenya 23,000 ,Bahrain ina 8,000, Oman 5,392, Kuwait 3,515, Iran 200, na Iraq 150.
Mudavadi hata hivyo alisema ni vigumu kutoa utambulisho wa watu hao kwa sababu baadhi yao hawajajisajili na misheni za Kenya.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































