#Local News

WANNE KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSU MAUAJI YA OJWANG

Washukiwa 3 waliokuwa wakizuiliwa katika kituo cha polisi cha Central wakati wa kifo cha bloga Albert Ojwang’ wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo, baada ya kukamatwa na maafisa wa IPOA hapo jana kwa madai kwamba walitumiwa na polisi kumtesa bloga huyo kabla yao kuachiliwa katika mazingira yasiyoeleweka.

Mwingine anayetarajiwa mahakamani hii leo ni OCS wa kituo hicho Samson Taalam, huku maafisa 2 walioonekana kwenye kanda za video wakipeleka mwili wa Ojwang katika hospitali ya Mbagathi wakiendelea kusakwa.

Haya yanajiri huku familia ya bloga huyo ikiendelea kushikiza haki.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *