TETESI ZA SOKA ULAYA
Real Madrid wameanza mpango wa kumsajili mchezaji wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, 25, kwenye dirisha la uhamisho la Januari ijapokuwa Liverpool wanapania kuongeza mchezaji huyo mkataba wa misimu miwili ili kusaidia katika kubeba mataji.
Mpango wa Real Madrid wa kumsajili beki huyo wa Uingereza, kwa uhamisho wa bure msimu ujao wakati mkataba wake na Liverpool utakapokamilika sasa umemweka mchezaji huyo katika nafasi tatanishi ya kufanya uamuzi. Usajili huu unakuja baada ya beki wa Uhispania Dani Carvajal, 32, kupata jeraha baya la goti.
Liverpool kwa upande wao, wanaendelea na mazungumzo ya kandarasi ya mabeki wawili, wakiwemo Jarell Quansah, 21, na beki wa Ufaransa Ibrahima Konate, 25.
Hayo yakijiri, timu ya Manchester City wametenga pauni milioni 80 kwa usajili wa wachezaji katika dirisha la usajili la Januari baada ya baadhi ya wachezaji wa kbalu hiyo akiwemo Rodri ya kujeruhiwa.
Na kocha wa zamani wa Barcelona Xavi anapigiwa upatu sana na anahusishwa na timu ya Manchester United ikiwa Erick ten Hag ataondoka. Usimamizi wa timu ya Manchester United hivi karibu umekuwa mbioni kutoa uamuzi ikiwa watasalia na Erick ten Hag msimu ujao.
Hii ni baada ya timu ya Manchester United kukosa kubeba mataji msimu uliopita isipokuwa taji la FA.
Imetayarishwa na Ken Osoro
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































