GACHAGUA ATENGWA SERIKALINI

Baadhi ya viongozi wa eneo la mlima kenya wanadai kwamba kuna njama ya kumtenga naibu wa rais Rigathi Gachagua serikalini.
Wakiongozwa na gavana wa nyeri Mutahi Kaiga viongozi hao wamehapa kupinga mpango wowote wa kumshusha hadhi Gachagua ambaye wamemtaja kama kiongozi wa mlima kenya.
Hata hivyo hapo jana msemaji wa ikulu Husseni Mohamed alipuuzilia mbali madai hayo akisisitiza kwamba rais William Ruto na naibu wake wana uhusiano mwema kwa upande wake kiranja wa wengi katika bunge la kitaifa Sylvanus Osoro amewasuta viongozi wa mlima kenya wanaodai kwamba maslahi ya eneo hilo yamepuuzwa na serikali ya kenya kwanza.
Kulingana na Oroso eneo hilo halifai kulalamika kiwa kuwa limetengewa nafasi nyingi serikali.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































