KATIBU MKUU WA KUPPET AKELO MISORI AKASHIFU WANACHAMA WANAOMSHUTUMU KWA USALITI

Katibu Mkuu wa Muungano wa sekondari na vyuo vya kadri (KUPPET) Akelo Misori ameshikilia kuwa kusitishwa kwa mgomo wa walimu siku ya Jumatatu sio uamuzi wake mwenyewe, bali uamuzi wa chama cha wafanyakazi.
Misori, ambaye ameshutumiwa kwa usaliti na baadhi ya wanachama wakuu wa KUPPET amesema wanachama hao ni wanafiki.
Ameongeza kuwa walisitisha mgomo huo wakiwa baraza kuu baada ya kushauriana kwa mapana na wajumbe na baada ya Tume ya Utumishi wa Walimu TSC kukubali kukidhi matakwa yao.
Imetayarishwa na Janice Marete