MCHUANO MKALI WA OLYMPIKI

Ufaransa itakutana na Argentina kwa mechi inayoweza kuwa na kinyongo mjini Bordeaux katika mechi ya robo fainali ya Olimpiki ya wanaume hapo kesho.
Hivi majuzi kumekuwa na uhasama kati ya timu hizo baada ya wachezaji wa Argentina kurekodiwa wakiimba wimbo wa dharau kuhusu wachezaji weusi wa Ufaransa baada ya kutwaa ubingwa wa Copa America tarehe 14 Julai.
Ilikuwa sawa na wimbo ulioimbwa na mashabiki wa Argentina wakati wa Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar – mashindano ambayo Argentina iliishinda Ufaransa katika fainali.
Katika Olimpiki, wachezaji wa raga ya wachezaji saba wa timu ya taifa ya Argentina walizomewa katika kila mchezo wao na mashabiki wa Ufaransa huko Paris, na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta anafikiri mechi ya kesho inaweza kuvutia hisia kali zaidi kutoka kwa mashabiki wa wenyeji Ufaransa.
Imetayarishwa na Nelson Andati