UCHUNGUZI WA AJALI YA KWAMBIRA WAANZA, WATU 3 WAFARIKI
Uchunguzi umeanza kufuatia ajali iliyotokea katika eneo la Kwambira, barabara ya Nairobi-Nakuru, ambapo watu watatu wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.
Ajali hii inafuatia nyingine ya wiki iliyopita katika eneo hilo ambapo watu watano walikufa baada ya gari lao kupoteza mwelekeo.
Polisi wamewataka madereva kuwa waangalifu na kufuata sheria za trafiki ili kuepuka ajali zaidi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































