HUDUMA KENYA YATAKIWA KUPIGA JEKI MIRADI YA SERIKALI
Idara ya huduma Kenya imetakiwa kupiga jeki juhudi za serikali kuhakikisha kuwa wakenya Zaidi wanajisajili kwenye bima ya Taifa Care.
Akizungumza kwenye kongamano la mameneja vituo vya Huduma Center jijini Mombasa, katibu katika wizara ya utumishi wa umma Amos Gathecha ameitaka idara hiyo pia kuorodhesha idadi ya wakenya waliosajiliwa kupitia huduma Kenya.
Aidha, ametoa hakikisho kuwa changamoto za vifaa vya kidijitali zitaondolewa hivi karibuni kwenye idara hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































