SHA YAZINDULIWA RASMI

Wizara ya afya imezindua rasmi mpango mpya wa afya katika maeneo mbali mbali nchini huku usajili wa wakenya kwenye mpango huo ukiendelea.
Katika kaunti ya Kakamgea, uzinduzi huo umeongozwa na Waziri wa afya Deborah Mulongo, ambaye amewahakikishia wakenya kwamba muda wa kusajiliwa utaongezwa.
Aidha, amewahimiza wakenya kujisajili kwenye mpango huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa