MKATABA WA SERIKALI-ADANI MAHAKAMANI
Mahakama imeipa serikali hadi tarehe 1 mwezi Agosti kuwasilisha Ushahidi kwamba kampuni ya KETRACO ilifutilia mbali mkataba wake na kampuni ya Adani ya usambazaji wa nguvu za umeme nchini.
Kwenye kikao cha kutajwa kwa kesi inayotaka Ushahidi huo kuwasilishwa, jaji Bahati Mwamuye aliarifiwa kuwa hilo halijaafikiwa, jaji Mwamuye akisema iwapo serikali haitafanya hivyo, basi kesi hiyo itasikilizwa kikamilifu.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 27 Oktoba mwaka huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































