POLISI WANASA PIKIPIKI 59 ZILIZOIBWA
Polisi mjini Eldoret wamewakamata watu wanne akiwemo mmiliki wa karakana baada ya kuwanasa na pikipiki 59 na sehemu 35 za injini zilizokuwa zimeibwa kutoka kwa wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Uasin Gishu.
Akiwahutubia wanahabari katika kituo cha polisi cha Central mjini humo, kamanda wa polisi Benjamin Mwathi amesema pikipiki hizo zimenaswa katika karakana eneo la Kapsoya baada ya kudokezewa na wananchi.
Aidha, amesema washukiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































