MWANGI APANGA TAMASHA UHURU PARK KWA KUHESHIMU WAANDAMANAJI WALIOFARIKI
Mwanaharakati Boniface Mwangi anapanga tamasha la wazi bila malipo katika bustani ya Uhuru Park kuwaenzi waandamanaji wote walioaga dunia kwa kupigwa risasi walipokuwa wakitekeleza haki yao ya kidemokrasia ya kupinga mswada wa fedha.
Alipokuwa akishiriki mipango hiyo katika mtandao wa X, Mwangi amesema juhudi za kumfikia Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja zimegonga mwamba. Mwangi ameongeza kuwa simu zake kwa gavana na Shaffie Weru, ambaye ndiye msimamizi wa hafla hiyo katika kaunti hiyo, hazikupokelewa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































