#Sports

ISRAEL WATUA PARIS

Wawakilishi wa Olimpiki wa Israel walisafiri kwa ndege kuelekea Paris siku ya Jumatatu huku kikosi cha Palestina kikitoa wito wa kuwapiga marufuku wachezaji wa Israel kutokana na vita vya Gaza.

Michezo hiyo itaanza Ijumaa hi dhidi ya hali ya wasiwasi mkubwa wa usalama na kuongezeka kwa hasira ya kimataifa juu ya idadi ya vifo na mgogoro wa kibinadamu unaoendelea Gaza.

Kamati ya Olimpiki ya Palestina ilisema Jumatatu ilituma barua kwa Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach, ikimtaka apige marufuku Israel, ikitaja mashambulizi kwenye ukanda wake kama ukiukaji wa makubaliano ya Olimpiki.

Barua hiyo “ilisisitiza kwamba wanamichezo wa Palestina, haswa wale wa Gaza, wananyimwa kupita salama mipakani na wameteseka sana kutokana na migogoro inayoendelea”.

Kabla ya safari ya kuelekea Ufaransa, Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Israel Yael Arad alisema “ni ushindi” kwamba wanamichezo 88 wa timu hiyo watashiriki katika Michezo hiyo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ISRAEL WATUA PARIS

WANA BUNDUKI WAKO MBIONI KUMSAJILI RICCARDO

ISRAEL WATUA PARIS

MULILI AIGURA  INGWE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *