GAVANA MUTAI ABANDULIWA

Gavana wa Kericho Eric Mutai amebanduliwa kutoka mamlakani na wawakilishi wa kaunti hiyo, hatma yake sasa ikiwa mikononi mwa bunge la seneti ambako atafika kujitetea.
Kubanduliwa kwake kumejiri kutokana na madai ya ukiukaji wa katiba, matumizi mabaya ya afisi yake na ufujaji wa raslimali za umma.
Hoja ya kubanduliwa kwake imeungwa mkono nawawakilishi wadi 31.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa