#Local News

MAUAJI KWARE: WANAHARAKATI WAIKOSOA SERIKALI

Huku visa vya mauaji dhidi ya wanawake vikiendelea kuongezeka nchini na serikali kushinikizwa kuwajibika, wanaharakati wameikosoa serikali kuhusiana na jinsi imeshughulikia mauaji ya wanawake ambao miili yao iliopolewa kutoka timbo ya Kware mwezi Julai jijini Nairobi.

Katika kikao na wanahabari, wanaharakati wameikosoa serikali kwa madai ya kushindwa kuwatambua waathiriwa na familia zao, wakihusisha hatua hiyo na idai ya juu ya miili ambayo haijatambuliwa katika makafani ya City.

Aidha, wametaka kukamatwa mara moja kwa mshukiwa mkuu wa mauaji hayo Collins Khalusia aliyetoroka kutoka kituo cha polisi cha Gigiri.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAUAJI KWARE: WANAHARAKATI WAIKOSOA SERIKALI

BALOZI WHITMAN AJIUZULU

MAUAJI KWARE: WANAHARAKATI WAIKOSOA SERIKALI

NAIBU GAVANA WA KAUNTI YA UASIN GISHU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *