WAKULIMA WA MIWA WAPINGA ‘KUVURUGIWA UTAMU’
Kundi la wakulima wanaouza miwa yao katika kiwanda cha Nzoia kaunti ya Bungoma wamepinga vikali maandamano yaliyopangwa na viongozi wanaopinga kukodishwa kwa kiwanda hicho kwa mwekezaji wa kibinafsi, wakiwataja viongozi hao kama wabinafsi.
Wakizungumza na wanahabari mjini Webuye, wakulima hao wakiongozwa na David Opala, uwepo wa kiwanda hicho chini ya serikali hakujawafaidi kwa muda mrefu, na hivyo kukodishwa kwake ni afueni kwao.
Aidha, wameelezea matumaini ya kupatikana kwa ajira kwa vijana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































