#Local News

UBONGO WA MCHUUZI KARIUKI WAFA

Familia ya mchuuzi wa maski Boniface Kariuki aliyepigwa risasi katikati mwa jiji la Nairobi imeingiwa na hofu, baada ya madaktari katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kutangaza kwamba ubongo wa Kariuki umekufa, ikimaanisha hauwezi kufanya kazi tena.

Ikiongozwa na msemaji wake Emily Wanjira, familia hiyo imeonyesha kutamausha, huku ikiomba msaada kuhusu bili ya hospitali ambayo sasa ni zaidi ya shilingi milioni 3.

Kitabibu, ubongo kufa inamanisha shughuli muhimu kama vile mapigo ya moyo na kupumua zimesimama.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *