GAVANA MWANGAZA ‘AKATAA’ KUENDA

Uamuzi wa kumbandua kutoka mamlakani gavana wa Meru Kawira Mwangaza umezua mkanganyiko wa kisheria, baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kumzuia spika wa seneti Amason Kingi kutochapisha tangazo la afisi ya gavana wa Meru kuwa wazi kwenye gazeti rasmi la serikali hadi kesi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Hata hivyo, agizo la jaji Bahati Mwamuye limejiri wakati ambapo tayari Spika Kingi amechapisha kwenye gazeti rasmi la serikali uamuzi wa bunge hilo kudumisha uamuzi wa bunge la kaunti ya Meru wa kumbandua Mwangaza.
Huku mahakama ikisubiriwa kutoa uamuzi wake, wakili wa masuala ya katiba Peter Wanyama, amasema kwamba kutokana na agizo la mahakama, Mwangaza ataendelea kuwa gavana hadi kesi yake itakaposikilizwa tarehe 17 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa