#Football #Sports

GOR MAHIA WACHARAZA ELMEREIKH BENTU YA SUDAN KUSINI 5-1

Timu ya kenya Gor mahia imeicharaza Elmereikh Bentu ya Sudan Kusini mabao 5-1 katika mechi ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika ya CAF kwenye Uwanja wa Nyayo na kujipatia tiketi ya

Kocha mkuu wa Gor Mahia Leonardo Neiva anasema wanapaswa kusalia wanyenyekevu na kuwa watulivu licha ya kuicharaza Elmereikh Bentu

Baada ya kufungwa 1-0 ugenini na Wasudan hao mjini Juba, K’Ogallo ilivuka kwa jumla ya mabao 5-2 na kujiweka sawa na wababe wa Misri, Al Ahly, ambao ni mabingwa watetezi katika raundi ya pili mwezi ujao na kocha Neiva anaamini kuwa kazi ipo.

Mbrazil huyo alisema wapinzani wake waliahidi kuwafunza Gor masomo ya soka. “Hii ndiyo sababu baada ya kufunga bao la kwanza, walijaribu mchezo wao wa kupoteza muda lakini KO’gallo aliwapata usingizini ili kubadilisha hali hiyo

Leonardo Aliahidi kujaribu kucheza mchezo mzuri dhidi ya Al Ahly bila kujiweka wazi.

Imetayarishwa na Janice Marete

GOR MAHIA WACHARAZA ELMEREIKH BENTU YA SUDAN KUSINI 5-1

NDANGIRI ANAAPA KUNYAKUA TAJI LA PILI LA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *