#Rugby #Sports

KOYONZO WATAREJEA KWA KISHINDO ASEMA KOCHA OKWEMBA

Kocha mkuu wa mchezo wa raga wa wachezaji saba wa Shule ya Sekondari ya Koyonzo Eliud Okwemba ameahidi kurejea kwa kishindo katika Michezo ya Mpira wa Shule za Sekondari Kanda ya Magharibi baada ya kushindwa kutetea taji lao la kaunti.

Okwemba anasema kokosa kujiamini miongoni mwa wachezaji wake na ulinzi duni nido  sababu za kushindwa kwao dhidi ya Shule ya Upili ya Wavulana ya St. Peter’s Mumias katika nusu-fainali.

Okwemba alisema wapo katika harakati za kujijenga upya kufuatia kuondoka kwa wachezaji wao wengi kwenye kikosi chao kilichotwaa ubingwa na kuwabakiza wachezaji wawili pekee.

Okwemba ana nia ya kuwashinda vigogo wengine wa eneo kama vile Shule ya Upili ya Kakamega, Butula na washindi wa pili wa Shule ya Upili ya Vihiga mwaka jana ili kuhifadhi taji lao.

Kakamega, mabingwa wa kitaifa wa 2013, waliwazaba St. Peter’s Mumias 12-5 na kunyakua taji la Kaunti ya Kakamega, huku Vihiga wakiishangaza Senende 22-0 kuhifadhi taji la Kaunti ya Vihiga.

Butula, vigogo wa Kaunti ya Busia, watalazimika kusubiri baada ya mechi za raga ya wachezaji saba saba za kaunti ya Busia kuahirishwa hadi tarehe iliyofuata.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *