#Local News

WAKULIMA WA MIWA MIGORI WATAKA WASAGAJI KUWA NA MIPANGO BORA YA MALIPO

Katibu wa Shirikisho la Kitaifa la Wakulima wa miwa Kenya tawi la Migori Argwengs Adongo ametoa wito kwa wasagaji wanaopata miwa kutoka kwa wakulima wa kaunti ya Migori kubuni mpango bora wa malipo kwa wakulima hao, la sivyo hawatapata miwa.

Adongo ambaye amepongeza serikali ya kitaifa kwa kuondoa malimbikizo yote ya wakulima amesema wasagaji lazima sasa wahakikishe kuwa wanalipa wakulima ndani ya muda wa wiki moja ya wiki mbili kutoka siku ya utoaji wa miwa.

Ameongeza kuwa ni lazima wasagaji wahakikishe malipo hayo yanafanyika mara moja na kuongeza kuwa hawataruhusu wasagaji kulimbikiza madeni tena

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *