KINERO NDO KOCHA WA MOMBASA UNITED.
KLABU iliyopewa jina jipya, Mombasa United imemteua Swaleh Kinero Ali kama kocha mkuu mpya.
Kinero anarejea katika usimamizi baada ya kuinoa Harambee Sand Stars katika Michezo ya Ufukweni ya Afrika Juni mwaka jana.
Alikuwa sehemu ya timu ya Coast Talanta Hela iliyopewa sifa kwa kuibua vipaji vipya kama Amos Wanjala, William Gitamu, Abdulhafidh Abdallah, na Ali Zambia.
Kinero ndiye aliyeiongoza Coast Stima kupanda daraja na atainongoza Mombasa United katika uwanja wa Mombasa Sports Club baada ya kubadili jina kutoka Mombasa Elite.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mombasa United Nick Arunga HUKU Katibu Mkuu wa klabu hiyo akiwa Alamin Wemalo.
Mombasa united inaanza msimu wao kwa safari ya kuelekea APS Bomet mnamo Septemba 7.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































