WAFANYIBIASHARA WA SOKO LA NAVAKHOLO KAKAMEGA WASUSIA KULIPA USHURU

Huenda Shughuli za Ununuzi na uchuuzi katika soko la Navakholo zikatatizika iwapo serikali ya kaunti ya Kakamega itafunga soko hilo kufuatia wafanyibiashara katika soko hilo kukosa kulipa ushuru.
Wafanyibiashara wa soko hilo wameapa kutolipa ushuru iwapo matakwa yao ya kutaka kujengewa vyoo, kusambaziwa maji na vile vile kuboreshwa kwa miundo msingi ya soko hilo hayatatekelezwa.
Kwa mujibu wa wafanyibiashara hao wanapitia hali ngumu wanapoendesha biashara zao za kila siku haswa wanapotafuta huduma za kimsingi kama vile maji na vyoo.
Wafanyibiashara hao sasa wanamtaka gavana wa kaunti hiyo Fernadez Barasa kuingilia kati na kuhakikisha wizara husika inawajibikia swala hilo kikamilifu.
Imetayarishwa na Janice Marete.