#Local News

NETANYAHU, HAMAS KUWASILISHWA ICC

Mwendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC Karim Khan, ameitaka mahakama hiyo kutoa amri ya kumkamata waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na viongozi wakuu wa kundi la kigaidi la Hamas kukabiliwa mashtaka ya kivita.

Akitoa hoja zake, Khan amesema Netanyahu na viongozi wa Hamas ambao ni Yahya Sinwar, Mohammed Diab Ibrahim na Ismael Haniyeh wametekeleza mauaji ya halaiki, kuwakamata mateka, ubakaji, dhuluma pamoja na matukio mengine ya kinyama.

Shirika la Habari la BBC limeripoti kwamba Khan anaamini ana ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashtaka.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

KIONI AWASUTA WAKOSOAJI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *