#uncategorized

WAIGURU: MAGAVANA WA KIKE SHARTI WAONGEZEKE

Mwenyekiti wa baraza la magavana ambaye pia ni gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, amewataka wanawake nchini kutotamaushwa na juhudi za mara kwa mara za kumbandua kutoka mamlakani gavana wa Meru Kawira Mwangaza, akisema kama magavana wa kike, wanalenga kuongeza idadi yao kutoka 7 hadi angalau 24 kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza wakati wa kongamano na magavana wa kike maarufu kama G-7 jijini Nairobi, Waiguru amewataka akina mama walio na ari ya kuwania wadhifa huo kusalia imara.

Magavana hao wametangaza kumuunga mkono Mwangaza katika kipindi hiki ambako hatma yake imo mikononi mwa bunge la seneti.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAIGURU: MAGAVANA WA KIKE SHARTI WAONGEZEKE

MAHAKAMA YAHARAMISHA NYONGEZA YA KODI

WAIGURU: MAGAVANA WA KIKE SHARTI WAONGEZEKE

MASTAA WA OLIMPIKI WATUZWA FEDHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *