SOKA YA KENYA YAOMBOLEZA KIFO CHA MWENYEKITI WA MATHARE UNITED BOB MUNRO
Mkurugenzi Mtendaji wa Mathare United, Jacktone Obure, amethibitisha kifo Bob Munro mtaalamu wa soka ambaye alifariki asubuhi ya jana Jumapili nyumbani kwake huko Westlands, Nairobi.
Munro anahusishwa na kuongoza moja ya mashirika makubwa ya soka nchini Kenya, ambalo limetengeneza mamia ya wachezaji bora wa soka. Mnamo Disemba 12, 2024, wakati wa sherehe za Siku ya Jamhuri, Rais William Ruto alimtunuku Munro tuzo ya Elder of the Order of Burning Spear (EBS) kwa mchango wake katika nyanja nyingi, si tu soka.
Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Hussein Mohammed, amemwomboleza Munro, akikumbuka michango yake kubwa katika maendeleo ya soka nchini. Vilevile, FKF kama taasisi imemwomboleza Munro, akitaja shauku yake kwa soka la vijijini.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































